BANDA MEDIA BLOG

CCM Z’BAR YAENDELEA KUFANYA UHAKIKI WA MALI ZAKE.


indexNa Is-haka  Omar, Zanzibar.
——————–
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  kimewataka wananchi wanaoishi katika maeneo yanayomilikiwa na chama hicho kuhakikisha wanafunga mikataba rasmi ili kuepuka usumbufu wakati  maeneo hayo yatakapohitajika kwa ajili ya shughuli za kichama.
Kimesema kuna baadhi ya wananchi waliopewa  maeneo ya kuishi kwa muda kwa nia ya kuwasaidia na badala yake wameyageuza kuwa makaazi yao ya kudumu jambo ambalo sio sahihi.

Akizungumza  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Vuai Ali Vuai kwa nyakati tofauti katika mwendelezo wa ziara ya kuhakiki mali na maeneo mbali mbali yanayomilikiwa na CCM huko Mbweni Mkoa wa Magharibi Kichama.
Alisema chama kinaendelea na zoezi la kuhakiki mali zake kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wanaotengeneza hati na mikataba  bandia ya kujimilikisha mali za chama hicho kinyume na utaratibu.
Ndg. Vuai alifafanua kwamba katika hatua za kupunguza kero hizo chama kimeamua watu wote ambao wamepewa kibinadamu sehemu za kuishi ama kufanya biashara kwa muda katika maeneo yanayomilikiwa na CCM wafunge mikataba rasmi ili chama kiweze kunufaika na rasilimali zake.
“ Watu waliopewa kwa dharura sehemu za kuishi na kufanya biashara kama hatujawapa  mikataba rasmi inayotambulikana kisheria, ambayo ni kielelezo cha kumtambulisha  nani  mmiliki halali wa maeneo hayo baadae inaweza kuwa fursa ya kufanya utapele na kusababisha usumbufu na lawama kwa chama. 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG