———————————————————
Na. Immaculate Makilika, MAELEZO
RAIS
wa Serikali ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame amewakabidhi tuzo kwa
Wizara, taasisi za Serikali, kampuni, nchi washiriki pamoja na mashirika
yaliyoshinda katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa.
Rais
Paul Kagame alikabidhi tuzo hizo jana, wakati alipokuwa akifungua
maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwl Nyerere
maarufu kama Sabasaba, vilivyopo katika barabara ya Kilwa jijini Dar es
salaam.
Wizara
na taasisi za Serikali, kampuni pamoja na mashirika mbalimbali
yalishiriki maonesho hayo kwa kushindana katika kuonesha bidhaa bora na
kueleza huduma nzuri wanazotoa, ambapo baadae Rais Paul Kagame
aliwakabidhi washindi hao tuzo mbalimbali.
Baadhi
ya washindi hao walioganywa katika makundi mbalimbali ni pamoja na,
kundi la bidhaa za kilimo nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na
kampuni ya farm equip Tanzania limited, nafasi ya mshindi wa pili
ilishikwa na kampuni Asas dairies na nafasi ya mshindi wa kwanza
ilishikwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA
JKT).
Katika
kundi la usindikaji wa vyakula na huduma za vinywaji, nafasi ya mshindi
wa tatu ilishikwa na kampuni ya Bakhresa Group, ikifuatiwa na kampuni
ya P&P, na nafasi ya mshindi wa kwanza ilishikwa na kampuni ya
Afri tea and coffe blenders limited.
Kwa
upande wa taasisi za kifedha, nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na
benki ya TIB, ikifuatiwa na Benki ya CRDB huku Benki Kuu ya Tanzania
(BOT) ikishika nafasi ya kuwa mshindi wa kwanza. Vilevile katika kundi
la Mifuko ya hifadhi ya jamii nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na
mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, nafasi ya mshindi wa pili
ilishikwa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF na nafasi ya mshindi wa kwanza
ikiwa ni Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Kwa
upande wa nchi za kigeni zilizoshiriki maonesho hayo ya 40 tuzo
zilienda kwa nchi za Rwanda iliyoshika nafasi ya mshindi wa tatu,
Ujerumani ikishika nafasi ya mshindi wa pili huku nafasi ya mshindi wa
kwanza ikiwa ni nchi ya Afrika Kusini. Aidha, washindi wa jumla
walioshiriki katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba
ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kilichoshika nafasi ya mshindi
wa tatu , ikifuatia Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja Chuo cha Cha
Ufundi Stadi (VETA) kilichoshika nafasi ya mshindi wa kwanza.
Baada
ya kuwakabidhi tuzo hizo na kufungua rasmi maonesho hayo ya 40 ya
biashara ya kimataifa Rais Kagame alitoa wito kwa washiriki wa maonesho
hayo ya 40, kushirikiana ili kubuni mawazo mapya ya biashara ikiwa ni
pamoja na kutambua fursa zilizopo katika soko la pamoja la Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, katika kukuza biashara zao na kusaidia ukuzaji wa
uchumi wa pamoja katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Tags
BIASHARA