Ndege ya pili ya Bombadier Q400
iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL)
ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe
za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano
Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400
iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL)
ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za
uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano
Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400
iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL)
ikiegeshwa karibu na pacha wake iliyofika wiki moja uliopita katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi
rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016
hapo hapo uwanjani.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard
Chamriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya
Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege
la Taifa (ATCL) ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea
Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo
umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard
Chamriho akisalimiana na Rubani John Kuipers aliyeeendesha Ndege ya
pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la
Ndege la Taifa (ATCL) na kuiwasilisha salama katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017
ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo
umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo
uwanjani.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard
Chamriho akikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na
serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard
Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus
Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika Ndege ya pili ya
Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege
la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea
Canada ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard
Chamriho na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi
wakitelemka baada ya kuikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400
iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL)
mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada
ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard
Chamriho akimpa pongezi Rubani John Kuipers aliyeendesha
aliyeendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali
kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Marubani John Kuipers na
Owen Davies walioendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa
na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) wakifurahia
mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada
ilikotengenezwa.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………….
Ndege mpya ya PILI iliyonunuliwa
na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar
es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Dash
– 8 Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:50 Mchana na kisha kupatiwa
heshima maalum kwa kumwagiwa maji na magari ya zimamoto (Water Salute).
Akizungumza baada ya kuwasili kwa
ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema baada ya
kuwasili kwa ndege zote mbili uzinduzi rasmi utafanyika kesho Jumatano
kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt.Chamriho amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi amesema ATCL
imejipanga kuingia katika soko la ushindani na kuwaahidi watanzania
huduma nzuri na bora katika kuhakikisha wanasafiri kupitia sekta hiyo ya
anga,kwa usalama na bei nafuu.
Ndege hii ya pili imewasili ikiwa ni wiki moja baada ya ndege ya kwanza iliyowasili tarehe 20 Sept 2016.
Tags
BIASHARA