Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 29 kupitia kwa mshambuliaji ghali Tanzania Obrey Chirwa kwa kichwa akipokea krosi safi toka kwa winga ya kulia Simon Msuva na kupelekea timu hizi ziende mapumziko wageni wakiwa mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa Toto kutaka kusawazisha bao kwa mabingwa hao ila bahati haikuwa yao kwani walijikuta wakitandikwa la pili dakika ya 55 kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya Kaseke kuangushwa ndani ya 18 na mwamuzi kuamua mita kumi na nane.
Hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Yanga wameibuka na ushindi wa magoli 2-0 na kuchupa nafasi ya pili wakiwa na pointoi 18 sawa na Kagera Sugar na kesho watasafiri kuwafuata Kagera Sugar mchezo ukitarajiwa kuchezwa uwanja wa Kaitaba Jumamosi ikiwa ni mwendelezo wa Ligi.
Ligi hiyo inatarajia kuendelea
tena kesho kwa Vinara wa Ligi hiyo wekundu wa msimbazi watakuwa kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kucheza na timu ya Mbao FC toka
jijini Mwanza.
Tags
MICHEZO KITAIFA