Kiongozi machachari kutoka chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha
Economic Freedom Fighter – EFF Bw. Julius Malema ni mmoja wa viongozi
wanaotarajiwa kuwasili nchini kuhudhuria mkutano utakaondaliwa na chama
cha upinzani cha ACT Wazalendo.
Mkutano huo unalenga kujadili mustakbali wa lililokuwa Azimio la Arusha.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam; Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa ACT Wazalendo Bw. Ado Shaibu ametaja vyama vingine
vilivyoalikwa na ambavyo viongozi wake wanatarajiwa kuwasili nchini kuwa
ni chama cha Labour cha nchini Uingereza, Die Link cha nchini Ujerumani
na Syriza kutoka nchini Ugiriki.
Shaibu amesema wakiwa nchini, viongozi hao watashiriki mjadala mpana wa
maudhui ya lililokuwa Azimio la Arusha ambalo hivi karibuni ACT
Wazalengo imeliibua upya na kuliita Azimio la Tabora, ambayo kimsingi
maazimio yote yanazungumzia ujenzi wa jamii inayochukia rushwa na aina
zote za unyanyasaji huku ajenda kuu ikiwa ni ujamaa na utaifa kwanza.
Tags
SIASA
