Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimesema muendelezo wa
kukamatwa kwa viongozi wa chama hicho hakuwayumbishi bali kunawajenga
kisiasa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amezungumza na waandishi wa
habari na kueleza kuwa suala hilo halitachukua muda mrefu kwenye
utekelezaji.
"Hapa tunapoongea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, Misiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi," amesema Dk Mashinji.
Amesema Watanzania wanapaswa kukemea suala hilo kwa kupaza sauti zao zifike mataifa mbalimbali wafahamu ukiukwaji wa sheria.
Tags
SIASA
