Wafanyakazi wa kampuni ya ORICA pamoja na watumishi wa kituo cha afya cha nyakumbu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha nyakumbu ,Abdallah Amiry Kiroboto akishukuru baada ya kupokea msaada huo.
Msimamizi mkuu wa kituo cha ORICA
Mkoani Geita,Yahya Ruyaga akimkabidhi Mganga mfawidhi wa kituo cha
afya cha nyakumbu ,Abdallah Amiry Kiroboto
…………………………………………………………………………………………..
IMEANDALIWA NA www.madukaonline.Blogspot.com
Kampuni ya ORICA ambayo
inafanya kazi za kulipua miamba ya dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa
Geita(GGM) na Buzwagi Imetoa vifaa tiba kwenye kituo cha afya cha
Nyakumbu kilichopo kwenye kata hiyo wilaya na Mkoa wa Geita vyenye
thamani ya shilingi Milion mbili(2000,000.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano hayo ,Msimamizi msaidizi wa kituo cha Orica mwandisi
Pascal Malugu,amesema kuwa walifikiria kuwa sio vyema kwenye jamii
ambayo wanafanyia kazi kutokutoa mchango wowote ambao utasaidia jamii
hivyo wakaguswa na kuamua kutoa vifaa tiba ambavyo vitasaidia kutoa
huduma za kiafya huku akitoa wito kwa makapuni mengine kujitolea misaada
mbali mbali.
“Si mara ya kwanza katika jamii
kutoa misaada kwani tulishawahi kutoa kifaa kingine cha Eqbet kwenye
hospitali ya Geita na sisi tuliona sio vyema kutotoa misaada ambayo
itasaidia jamii inayotuzunguka lakini niombe Mashirika na Makapuni
mengine kuguswa na kutoa misaada kwani hii ndio dini safi kuwasaidia
ambao ni wagonjwa”Alisema Malugu.
Hata hivyo kwa upande wake
msimamizi mkuu wa kampuni hiyo,Yahaya Ruyaga ameelezea kuwa wanaamini
kuwa msaada ambao wameutoa utapunguza adha iliyokuwepo kwenye kituo
hicho na kwamba ni mwanzo tu kwani wanajipanga kuendelea kutoa mchango
zaidi kwenye maeneo yaliyopo ndani ya Mkoa wa Geita.
“Sisi kama saiti ya Geita tulikaa
wafanyakazi na kuweza kufikiria kwamba je sisi kama sisi tunaweza
kufanya kitu gani kwenye jamii ili walau na sisi tuweze kuleta faida
kwenye jamii inayotuzunguka ndipo tulipoamua kuunda tume ya kufuatilia
vituo vyetu vya afya vilivyopo kwenye halmashauri ya mji mwisho wa siku
tukajua kituo cha Nyakumbu kina uhitaji mkubwa ndipo tulipoamua kutoa
msaada huu wa vifaa tiba”Alisema Ruyaga.
Aidha mganga mfawidhi wa kituo
hicho,Abdallah Amiry Kiroboto amesema kuwa vifaa walivyopatiwa
vitawasaidia kurahisisha kazi na kwamba kwa sasa wataweza kupima
magonjwa ya kisukari kutokana na kupatiwa kifaa hicho huku akiomba
msaada kwa wadau wengine kufika katika kituo hicho na kuwasaidia kwani
wana upungufu mkubwa wa vifaa vingi vya kufanyia kazi.
Baadhi ya wananchi ambao
walikuwepo kwenye makabidhiano hayo wameishukuru kampuni hiyo kwa moyo
wa kujitolea huku wakiomba makampuni ambayo yamo ndani ya mgodi wa GGM
kuiga mfano wa kampuni hiyo.
Tags
AFYA