Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
amesema kuwa chama hicho kina mpango wa kufungua Chuo Kikuu cha chama
hicho.
Akizungumza katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na Channel Ten
ambapo amesema chuo hicho kitatoa mafunzo kwa wanachama, makada na
viongozi wote wa chama na hata waliopo serikalini kupitia chama ili
kuwafundisha itikadi za chama hicho.
Alisema, “Unajua chama cha Mapinduzi na chama cha kikominist (Uchina) ni
marafiki, tumeamua tujenge chuo kikuu cha chama cha mapinduzi ambacho
kitakuwa na kazi ya kuwafundisha wanachama, makada,viongozi na wale
waliopata dhamana serikalini. Kupitia chama cha mapinduzi tutawafundisha
ili tuelewane itikadi yetu, watu hujiunga na chama si kwa ajili ya
ushabiki ila watu wanajiunga na chama kwa sababu wanaamini wameielewa
itikadi ya chama hiki ni nini.”
Tags
SIASA
