Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na
iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.
Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari
katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia
ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya
hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni linalodaiwa
serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya Zanzibar
kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.
Dkt. Shein katika mazungumzo yake na vyombo vya habari alilezea mkutano
huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema mkutano huo utaleta tija
na faida kubwa kwa wazanzibari na watanzania katika nyanja mbalimbali za
kiuchumi ikiwemo utalii,uvuvi,ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi
wa bahari.
Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao
ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya na ulihudhuriwa na marais wa
nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika
Afrika Kusini.
Tags
ZANZABAR
