Ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli ya kutatua kero ya maji kwa wakazi
zaidi ya 12,000 wa mji mdogo wa Kisesa wilaya ya Magu mkoani
Mwanza,hatimaye imetekelezeka ndani ya miezi miwili, baada ya mamlaka ya
majisafi na usafi wa mazingira jijini Mwanza ( MWAUWASA ) kutumia zaidi
ya shilingi milioni 62 kujenga mradi wa maji katika mji huo na hivyo
kumaliza kabisa kero ya maji ya muda mrefu.
Ujenzi wa mradi mpya wa maji Kisesa ulianza Januari 29 mwaka huu,siku 18
baada ya Rais john Magufuli, aliyekuwa akipita eneo la Kisesa akitokea
Chato kuelekea Bariadi mkoani Simiyu kuombwa na wakazi wa mji huo
awasaidie kutatua kero ya maji, ambapo alimuagiza Waziri wa maji na
umwagiliaji Mhandisi gerson Lwenge kuhakikisha anashirikiana na mamlaka
ya majisafi na usafi wa mazingira jijini mwanza ( MWAUWASA ) kutatua
changamoto hiyo iliyokuwa inawakabili wakazi wa kisesa.
Mkuu wa wilaya ya Magu Bi.Hadija Nyembo akizindua mradi huo amekemea
tabia ya baadhi ya wananchi kuihujumu MWAUWASA kwa kujiunganishia maji
bila kufuata taratibu,sambamba na wanaojihusisha na wizi wa dira za maji
na wanaoiba maji baada ya kusitishiwa huduma hiyo kutokana na madeni.
Baadhi ya wakazi wa eneo la Kisesa,wanaeleza jinsi walivyokuwa
wakitaabika kwa kukosa majisafi na salama kabla ya mradi huo kukamilika.
Tags
RAIS MAGUFULI
