Katibu wa Mbunge
Ridhiwani Kikwete, bw. Iddi Swala akizungumza na wakazi wa kijiji cha
Vigwaza kuhusu utekelezaji wa mfuko wa jimbo na Ridhiwani alivyosaidia
kijiji hicho na kata kijumla. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Katibu wa mbunge wa
Ridhiwani Kikwete, anaeitwa Iddi Swala akionyesha saruji waliochangia
ujenzi wa shule ya msingi Vigwaza. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mifuko 50 ya saruji
iliyochangiwa na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, na
mifuko 50 aliyochangia diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa sita shule ya msingi Vigwaza. (Picha na
Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Vigwaza
WAKAZI wa kijiji cha
Vigwaza,Kata ya Vigwaza,jimbo la Chalinze,wameanza kuchangia matofali
matano kila mmoja na kujitolea nguvu kazi ili kujenga vyumba vitano vya
madarasa na chumba kimoja cha chekechea katika shule ya msingi Vigwaza.
Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Ramadhani Kirumbi, alisema serikali ya kijiji imekubaliana na
wananchi kuongeza majengo shuleni hapo.
Kutokana na juhudi
hizo, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, alieleza
anatambua jitihada za wananchi hivyo atawaunga mkono kwa kuchangia sh.
Mil mbili.
Mhandisi Ndikilo,
alisema jamii ishirikiane na serikali kwa kutatua changamoto za kijamii
hasa elimu ili kuwajengea mazingira bora wanafunzi.
“Tulijikita kwenye
kuondoa matatizo ya uhaba wa madawati lakini kwasasa haina budi
tujiongeze kumaliza changamoto ya majengo na madarasa “alibainisha .
Nae mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, alichangia mifuko ya saruji 50 na mabati 50 yenye thamani ya mil. 1.9 .
Katibu wa mbunge huyo
Iddi Swala,alisema Ridhiwani amechangia pia zahanati ya kijiji kipya cha
Mnindi mifuko 50,ukarabati nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mnindi
mifuko 30.
Hata hivyo, Ridhiwani alitoa mifuko mingine 30 kwa ajili ya kufanya ukarabati zahanati ya Kitonga.
Katibu Swala, alieleza
kwamba, mh mbunge kapeleka mifuko ya saruji mingine 50 katika shule ya
msingi Milo na zahanati ya Buyuni ametoa mifuko 30 ya saruji.
“Kati ya fedha za jimbo mil 48 kata ya Vigwaza imechangiwa mil. tano “alisema Swala kwa niaba ya Ridhiwani.
Diwani wa kata
Vigwaza,Mohsin Bharwani, alitoa mifuko 50 ya saruji na taasisi ya lions
Dar es salaam -Panorama imesaidia mifuko ya saruji 50.
Bharwani alisema kwasasa, katika sekta ya elimu wanajikita kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa kwenye shule mbalimbali.
Tags
HABARI ZA DINI