Balozi mdogo wa China aliepo
Zanzibar Xie Xiaowu akimkabidhi Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit
Kombo msaada wa dawa uliotolewa na Serikali ya China makabidhiano haya
yamefanyika Bohari Kuu ya dawa Maruhubi Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu
wakisaini hati ya makabidhiano ya dawa zilizotolewa Serikali ya watu wa
China.
Wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa
Zanzibar na wanafunzi wa fani ya ufamasia wakifuatilia sherehe ya
kukabidhiwa dawa zilizofanyika Bohari Kuu ya Maruhubi.
Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa
Zanzibar Zahran Ali Hamadi akizungumza na wandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu kubore kwa hali ya dawa Zanzibar baada ya Waziri wa Afya
Zanzibar kukabidhiwa msaada wa dawa kutoka Serikali ya watu wa China.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo.
Tags
AFYA ZANZIBAR