Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu
wa Kanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat
Gwajima.
Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na
kupekuwa na kupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake
lililopo Ubungo.
“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi
kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi
tutajua nini cha kufanya,”amesema Kibatala.
Aidha Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema
“Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo, baada
ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa
dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana
taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.
Tags
SIASA
