Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu
za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na
waadishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa
mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu kutoka
Ofisi hiyo Hashim Njewele.
Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu
za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na
waadishi wa habari kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017
leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia maelezo kuhusu hali ya mfumuko wa bei kutoka kwa Kaimu
Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth
Minja (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi ha oleo
Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
………………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa
na huduma nchini Tanzania umeongezeka kwa kiasi kidogo ukilinganisha na
nchi za Afrika Mashariki.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja
wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth
Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa
bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari mwaka 2017.
Ruth amesema kuwa mfumuko huo
umeongeka kutoka asilimia 5.2 mwezi Januari hadi kufikia 5.5 mwezi
Februari, 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3 kiasi ambacho
hakina athari katika uchumi wa nchi.
“Ongezeko hilo la mfumuko wa bei
umeendelea kukua kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi zingine za
ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Uganda na Kenya ambazo
tunashabihiana kwa kiasi kikubwa”. Alisema Ruth Minja.
Kwa upande wa mfumuko wa bei kwa
bidhaa za Vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka,
umeongezeka hadi asilimia 9.3 kutoka asilimia 8.2 mwezi Januari, 2017,
wakati badiliko la fahirisi kwa bei zisizo za vyakula limebaki kuwa
asilimia 3.6 kama ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.
Ameongeza kuwa farihisi za bei
zimeongezeka hadi 106.97 mwezi Februari,2017 kutoka 101.44 mwezi
Januari, 2017 wakati mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji
baridi kwa mwezi Februarii,2017 zimeongezeka hadi asilimia 8.7 kutoka
asilimia 7.6 ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.
“Mwenendo wa fahirisi za bei za
Taifa na Mfumuko wa Bei kutoka mwezi Februari 2016 hadi mwezi Februari,
2017 umeendelea kuimarika ambapo katika kipindi hicho, mfumuko wa bei
umekuwa na mwenendo imara kutoka asilimia 5.6 mwezi Februari, 2016 hadi
asilimia 5.5 februari,2017,”alisema Kaimu Meneja huyo.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
kupitia Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inao wajibu na mamlaka ya
kuratibu upatikanaji na utoaji wa takwimu rasmi nchini..
Tags
HABARI KITAIFA