Malkia wa taarabu nchini Tanzania Khadija Kopa amesema kwa sasa
anajipanga ili aweze kufanya video tofauti na video za kawaida za muziki
huo.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Khadija amesema "Video tunazotaka
kuzitengeneza ni zile za kiwango cha juu ambazo kuna wadhamini ambao
watakaotudhamini ili tuweze kukaa kambini kwa siku mbili hadi tatu ili
kutengeneza video zenye kiwango cha juu na zakimataifa" Amesema Khadija
Khadija Kopa pia amesema bado yuko fiti katika fani hiyo huku akitumia
kauli ya "Ng'ombe hazeeki maini" na amelithibitisha hilo kwa mashabiki
zake kupitia show kali aliyoipiga siku ya jana katika ukumbi wa Hisaje
Park, Boko Magengeni DSM, akishirikiana na Young Killer.
Tags
KIBURUDANI
