Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Constantine Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufunga
mafunzo ya jumla ya wahitimu 74 waliopewa mafunzo ya siku tatu katika
maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na
upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu. Mafunzo hayo yaliandaliwa na
Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST Mkoani Mbeya, lengo likiwa ni
kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi
mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo
chini ya kiwango. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell
Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas
Mwiru (kulia)
Baadhi ya wahitimu waliohitimu
jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na
vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu
yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika
Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki
74.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha
Utalii,Jesca William akiwaonesha baadhi ya video zinazotumika katika
kutoa mafunzo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja
na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa
siku tatu.
Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo
katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja
na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu, Lyimo Leb akitoa neno la
shukrani kwa mgeni rasmi kabla ya mafunzo hayo kufungwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya,Constantine Mushi akizungumza na wahitimu kabla ya kufunga jana
mafunzo hayo fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa
siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya wahitimu 74. Wengine ni Mratibu wa
Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi
Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru (kulia) (P
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya,Constantine Mushi akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa wenye hoteli
katika mkoa wa Mbeya, Jeremiah Mchange cha ushiriki wa mafunzo katika
maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na
upishi
Mratibu wa Mradi wa SPANEST
nchini, Godwell Meing’ataki akizungumza na wahitimu waliohitimu jana
mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji
pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na
Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa
muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya
Utalii, Paskaz Mwiru akizungumza na wahitimu kabla ya kufungwa mafunzo
hayo jana katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na
vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu
yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika
Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki
74. (Picha na Lusungu Helela- WMU)
…………………..
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Constantine Mushi amewataka wamiliki wa hoteli kuajiri wafanyakazi wenye
ujuzi katika fani ya ukarimu na utalii baadala ya kuajiri ndugu zao
wasio na ujuzi wowote na kuwalipa ujira mdogo hali inayochangia
kuzorotesha huduma za utalii mkoani hapo.
Alisema wahudumu walio wengi
katika hoteli hizo wamekuwa kero katika utoaji wa huduma kwa watalii
pindi wanapotembelea kuja kuona vivutio vya utalii vilivyopo mkoani
hapo.
Ametoa raia hiyo jana wakati
akifunga mafunzo hayo kwa jumla ya wahitimu 74 yaliyoandaliwa na Wizara
ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST
unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Amesema mafunzo hayo
yamefanyika kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma
zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi mahitaji ya
soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya
kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Amesema Wahitimu hao wamepewa
mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji
pamoja na upishi kwa ufadhili wa asilimia 75 uliofanywa kupitia mradi wa
SPANEST
Aidha, Mushi alisema kwa
kutambua umuhimu wa sekta ya utalii tayari umejipanga katika kuboresha
sekta ya utalii ambapo kwa mkoa wa Mbeya imeshaandaa Mpango Mkakati wa
kuendeleza utalii .
Kwa upande wa Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru amesema mafunzo hayo yatakuwa
endelevu kwa wahudumu na pamoja na wamiliki wa hoteli ili waweze
kutambua umuhimu wa wafanyakazi wao.
Naye, Mratibu wa Mradi wa
SPANEST, Godwell Mengiaediek amewataka wahudumu wa hoteli waunde chama
chao ambacho kitawasaidia katika kupaza sauti zao.
Tags
HOTEL'S