BANDA MEDIA BLOG

WANAOFANYA UJASIRIAMALI KWENYE MIKUTANO IKIWEMO INAYOFANYIKA DODOMA WALALAMIKIA VITENDO VYA UKAHABA

Mjasiriamali Mary Naali toka Karatu mkoani Arusha akionyesha ubunifu wake kwa kutengeza nguo ya ndani ya wanawake kwa kutumia Shanga mjini Dodoma  ambako vikao vya CCM vikiendelea

Wajasiriamali wanaofanya biashara za shanga, nguo na viatu toka ndani na nje ya mkoa wa Dodoma wamesema wanakerwa na vitendo vya baadhi ya wenzao kuwadharirisha kwa kufanya biashara mbilimbli ikiwemo miili yao.

Mary Naali toka Karatu mkoani Arusha ambaye anauza shanga na mikoba alisema tabia ya wenzao hao ya kujirahisi kwa kuuza miili yao ili kusevu fedha za biashara zao zinawaweka katika wakati mgumu kwa kuwa wanaume walio wengi wanapomaliza kupatanisha bei ya bidhaa zao huomba namba za simu na kisha kuwataka kuzipeleka mahotelini walikofikia kwa lengo la kuwatongoza 


Nae Irene Mmali anayeuza nguo toka jijini Dar es saalam  alisema kuwa biashara yake imekuwa ikimuwezesha kufanya mambo mengi ya kimaendeleo ikiwemo kuweza kumlipia mtoto wake milion 1.2   shule hivyo wanapojitokeza makahaba na kujiingiza katika biashara hizo kwa lengo la kijipatia kipata kwa njia ya ngono inawahalibia waliopo kihali 

"haiwezekani wauza ngono wanatuhalibia unadhani waumetu wakisikia hayo si watajua sisi wote tunafanya uchafu huo nashauri kama kuna mamlaka ya kuweza kulifuatilia na kulikomesha hilo basi ifanye kwa kuwa wengine tunategemea vikao kama hivi vya kisiasa na vya kiserikali kuendeshea maisha yetu na ya familia"m alisema

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG