MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk
Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni wafanyabiashara wa Ufaransa
waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini.
Katika hafla hiyo ya chakula cha
usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa
makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa
nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji
nchini Zahiri Zoro.
Akizungumza kabla ya kukaribisha
wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema katika hoteli ya
Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara
hao kuamua kuja nchini kuwekeza.
Alisema jioni hii ya leo hana
maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao ambao ni
muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo
na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum
ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa
Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)
“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili.
Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni
miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania
kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na
uwezo pia.
Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi.
Aliwatakia wageni wake chakula chema.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa
maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es
Salaam.
Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi
wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na
ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki
ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano.
“ …Business and friendship goes Together..”
alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana
na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na
Tanzania si wa kubahatisha unakua.
Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa
Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni
mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa
wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye
‘cocktail’ kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa.Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Eng. Raymond Mbilinyi
(kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika halfa
ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwa wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo
na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga
katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini
Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.Mkurugenzi
wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi
‘Application’ ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga
(kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka
Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce
Mhaville.‘Meet
and Greet’ ikiendelea kwa wenyeji na wafanyabiashara kutoka makampuni
makubwa nchini Ufaransa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa
na Dk.Mengi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mwimbaji
mkongwe nchini Mzee Zahir Ally Zoro akitumbuiza kwenye hafla ya chakula
cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na
Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Meza
kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa
ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini,
Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja
na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye
akisherehesha wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara
kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk Mengi kwenye hoteli Serena jijini
Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi
Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati wa hafla ya chakula cha
usiku kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyofanyika usiku wa
kuamkia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha
juu na chini ni wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini
Ufaransa wakijumuika na wenyeji wao katika hafla ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE – Saccoss), Anna
Matinde alikuwa miongoni mwa wageni waaalikwa katika hafla hiyo.