Mwenyekiti wa Kamati
ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kiwango
kilichoonyeshwa na aliyekuwa kipa wao, Juma Kaseja ambaye kwa sasa
anaichezea Kagera Sugar, ni cha kawaida na kudai kuwa hajaona cha ziada
kwake.
Simba ilipoteza
mchezo wake wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar na kujikuta ikiwa nafasi
ya pili ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 55 nyuma ya Yanga yenye
pointi 56, huku kipa Kaseja akionekana kuwa kikwazo kutokana na umahiri
ambao aliuonyesha uwanjani.
Hans Poppe alifunguka
kuwa, kiwango kilichoonyeshwa na Kaseja katika mechi dhidi ya Kagera ni
cha kawaida kama alivyokuwa akicheza katika timu yao na kudai kuwa
hakuona cha ziada kutoka kwake.
“Ndiyo Kaseja alikuwa
mchezaji wetu na aliondoka katika timu yetu miaka kadhaa iliyopita,
vilevile amecheza katika timu mbalimbali, kwa upande wangu naona kiwango
ambacho amekionyesha katika mechi dhidi ya Kagera ni cha kawaida kama
vilevile alivyokuwa akicheza alipokuwa Simba na sijaona cha ziada kutoka
kwake, anacheza kama ilivyo kwa makipa wengine.
“Wachezaji wengi
wamekuwa wakiondoka na wanaonyesha viwango vya kawaida lakini mwisho wa
siku Simba inabakia kuwa ileile,” alisema Hans Poppe.
Tags
KASEJA