![]() |
| Charles Makongoro Nyerere akiuelezea moja ya mkataba wa Jumuiya ya africa mashariki na kati kwa wafanyabiashara wa Dodoma |
WAFANYABIASHARA mjini Dodoma wamesema wao siyo waoga
kufanya biashara nje ya nchi bali vikwazo vya upatikanaji wa vibali ni tatizo
kubwa linalowasababisha kushindwa
kufanya biashara katika nchi wanachama wa Africa mashariki na kati
Wafanyabiashara hao wameitoa kauli hiyo wakati
wakiongea na wabunge wa Bunge la Africa masahariki na kati ambao walifika mjini
humo kwa lengo la kupata changamoto zinazowakabili kiasi cha kushindwa kufanya
biashara zao nje ya mipaka ya Tanzania ambapo kwa upande wake Mtalemwa Mshaju
amesema watanzania siyo waoga
Nae Fred Mushi amewaomba wabunge hao kuwasaidia
wafanyabiara kuvusha mahindi kutoka nchini Uganda ili waweze kuwauzia
Watanzania kwa bei nafuu badara ya kuacha wajanja wachache kuingiza mahindi kwa
njia zisizo halali
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wabunge wa jumuiya
hiyo nchini Tanzania Adamu Kimbisa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mazungumzo
hayo yaliyojumuisha wafanyabiashara walio wanachama wa TCCIA amewataka
kuchangamkia frusa
Aidha mwenyekiti wa mazungumzo hayo Charles
Makongoro Nyerere amesema fursa zipo na wafanyabiashara wanatakiwa kuzichangamkia, huku akiwataka kujiamini kwa kutojiona wanyonge bali waingie katika ushindani kwa ubora wa bidha kama ilivyo kwa mataifa mengine
RIPOTI YA JOHN BANDA, DODOMA
Tags
WABUNGE WA EAC



















