![]() |
| Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson akishiriki mazoezi ya viungo na vikundi vya mazoezi vya Dodoma Fitness Jogging & Sports Club na Muungano Jogging, katika uwanja wa jamhuri mjini Dodoma |
![]() |
| Wanamazoezi wa makundi hayo wakishiriki mazoezi hayo yaliyofanyika jana kwa kufuata maelekezo ya walimu wao wanaofuatisha mdondo wa muziki |
![]() |
| PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG |

![]() |
| Mazoezi ya kupunguza tumbo [kitambi] yakiongozwa na Mawalimu Mussa wa Dodoma Fitness |
![]() |
| Dodoma Fitness Jogging Sports, Club wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi hayo |
Na John Banda, Dodoma
Naibu Spika Dk, Tulia Akson amewataka viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na watendaji wa serikali kushiriki mazoezi ili kuweza kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa na yale ya kuambukizwa
akiongea katika uwanja wa jamhuri mara baada ya mazoezi ya asubuhi Tulia alisema yeye amekuwa akishiriki mazoezi kila siku kwa kuwa yamekuwa yakichamsha mwili na akili hivyo kumrahisishia kufanya kazi zake bila kuchoka
"hivi sasa wabunge viongozi pamoja na watendaji wa serikali wapo Dodoma hivyo ningewashauri kushiriki katika mazoezi hapa uwanja wa jamhuri ili kuchangamsha mwili na akili lakini pia itawasaidia kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa na pia mtu akiwa bize na mazoezi hata hayo ya kuambukizwa hayatampata", alisema
aidha alisema ni vema kila mtumishi na wanadodoma kushiriki mazoezi hayo ili kuendelea kumuunga mkono Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyewaagiza watanzania kushiriki mazoezi walau kila jumamos ya pili ya kila mwezi
Tags
MICHEZO
















