
Rais wa Marekani, Donald Trump amekejeli jaribio la kombora la kinyuklia
la Korea Kaskazini lililofanyika jana, akidai kuwa ingawa limeshindwa
ni dharau kwa China.
Jana, Korea Kaskazini ilidai kufanya jaribio lake la kombora la Nyuklia
ambalo Marekani ilidai kuwa lilishindwa hata kuvuka mipaka ya nchi hiyo
ndani ya dakika chache tangu lilipofyatuliwa.
“Korea Kaskazini imedharau matarajio ya China na ni dharau ya hali ya
juu kwa Rais [wa China], ingawa limeshindwa, jaribio la makombora la
leo. Mbaya!,” Tafsiri isiyo rasmi ya Tweet ya Rais Trump.
Trump alisema kuwa angependa sana kuumaliza mgogoro wa makombora ya
kinyuklia wa Korea Kaskazini kwa njia ya kidiplomasia, lakini ni vigumu
sana kutumia njia hiyo.
Tags
Donald Trump