BANDA MEDIA BLOG

WAPINZANI WA YANGA CAF KUWASILI ALHAMIS HUKU MKWASA AKITAJA VIINGILIO CHA CHINI BUKU TATU


Mouloudia_dAlger
Na. Carlos Nichombe
WAPINZANI wa Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya MC Alger kutoka Algeria watawasili nchini kesho Kutwa kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao utafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jumamosi hii.

Msafara huo wenye watu 40 utawasili saa 3 usiku ambapo shughuli zote za timu hiyo zitasimamiwa na ubalozi wa Algeria hapa nchini.
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa wapinzani wao hao wamethibitisha kuwasili siku hiyo na kwa tahadhari kubwa huku wao wakiwa wamejipanga
vizuri kwa mchezo huo.
“MC Alger watawasili Alhamisi kwa ndege maalum kwa ajili ya mchezo wetu wa huo, kikosi chetu kilianza mazoezi jana Jumatatu na leo jioni Jumanne wataendelea,” amesema Mkwasa.
Ameongeza kuwa Timu hiyo inatarajia kuondoka siku ya Jumamosi saa 5 usiku mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao huo ambao unaelezwa kuteka hisia za mashabiki wa soka hapa nchini.
Pia Mkwasa ametoa sababu za kutaka kuamisha mchezo wao dhidi ya Mc Alger mkoani Mwanza kutokana na kutaka kutoa fursa kwa mashabiki wengine walio nje ya Jiji la Dar es Salaam kushuhudia michezo mingine ambayo hawajawahi kuishuhudia.
Amesema Yanga inaidadi kubwa ya Mashabiki pande zote za nchi na kuendelea kuweka michezo yote jijini Dar es Salaam kunawanyima fursa baadhi ya mashabiki na wanachama wao ambao hawana uweo wa kwenda uwanja wa Taifa kushihudia michezo hiyo.
Wakati huo huo, Mkwasa amevitaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni Sh 5000 kwa mzunguko, VIP B na C ni Sh 20,000 na Sh 30,000 kwa VIP A.
Amesema wameamua kuweka viingilio hivyo ili kupata pesa itakayowawezesha kusafiri kwenda kwenye mchezo wa marudiano nchini Algeria hivyo kuwataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG