BANDA MEDIA BLOG

YANGA YATOA UFAFANUZI JUU YA UJIO WA KOCHA MPYA


WhatsApp-Image-2017-02-27-at-03.33.31
Na.Alex Mathias,Dar es salaam
Uongozi  wa Klabu ya Yanga umekanusha vikali taarifa za kutaka kumsajili kocha wa AFC Leopards ya Kenya, Stewart Hall kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kocha George Lwandamina ambaye ilisikika
wanataka kumtupia virago.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na taarifa mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawakilishi wa Yanga walisafiri kuelekea nchini Kenya kufanya mazungumzo na Muingereza huyo ili
mwezi Juni ajiunge na mabingwa hao.
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa amedai taarifa hizo sio za kweli na zina lengo la kulichanganya benchi la Ufundi ili lishindwe kutimiza majukumu yake vizuri kwenye michezo iliyosalia
kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na Mashindano ya Kombe la Shirikisho.
Ameongeza kuwa wanaelewa lengo kubwa la watu waliotoa taarifa hizo za uongo ni kutaka kuwachanganya kati ya viongozi wa timu hiyo pamoja na benchi la ufundi ambalo linaweza kupoteza muelekeo wao kwa kile kitu walichokianza.
Amesema Uongozi wa Yanga hauoni tatizo lolote kwa Benchi la Ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mzambia George Lwandamina kwani amefanya kazi kubwa na ya maana katika kuhakikisha Yanga inarejea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
“Hizo taarifa ni uzushi mtupu hatuna mpango na Hall, tunaliamini benchi letu la ufundi na hatuko tayari kurudia makosa tuliyofanya nyuma,” alisema Mkwasa.
Ikumbukwe Hall aliwahi kuiongoza Azam FC miaka ya nyuma na kufanikiwa kuipa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara pamoja kombe la Kagame.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG