Wakandarasi hao 18 kati yao ni makampuni mawili tu amayo yanatoka katika kampuni kutoka nje ya nchi na wakandarasi kumi na sita ni makampuni kutoka ndani ya nchi(Wazawa).
Akizungumza na wakandarasi, wabunge, viongozi wa REA na viongozi kutoka TANESCO ,Waziri wa Nishati na Madini Prof; Sospiter Muhongo alisema miradi hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa muda mwafaka pamoja kutumia vifaa ambavyo vina ubora.
Prof.Muhongo amesema katika kutekereza mraji wa umeme vijijini wakandarasi wote wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata mikataba yao inavyowaelekeza sambamba na kupeleka umeme katika maeneo muhimu.
Ameeleza kuwa REA awamu ya pili iliweza kuruka maeneo mengi na kuwafanya wananchi kutopata huduma hiyo lakini kwa sasa REA awamu ya tatu inalazimisha kila sehemu muhimu kupatiwa umeme.
“Katika harakati za kusambaza umeme wakandarasi hakikisheni mnafikisha umeme katika maeneo muhimu sana ikiwa ni katika taasisi mbalimbali kama vile mashule,zahanati, vituo vya afya,makanisani na misikitini, pamoja na maeneo ambayo yanaonekana kuwa na mkusanyiko wa watu.
“Pia katika kusambaza umeme lazima kufikisha umeme hata kama ni sehemu ambayo ni kijiji kwa maana ya kuwepo kwa mazizi ya ng’ombe, mbuzi na makaburikwa kutambua kuwa iwapo wananchi hao watapatiwa umeme wataweza kuwa na maendeleo ili kutimiza sera ya serikali ya viwanda” amesema Prof .Muhongo.
Katika hatua nyingine Prof.Muhongo amewataka wakandarasi,watumishi kutoka REA , Wabunge pamoja na kuhakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza mpango wa kusambaza umeme vijiji bila kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.
Naye mkurugenzi wa Wakara wa Umeme Vijijini,Mhandisi Bengiel Msofe amesema katika kutekeleza miradi hiyo wakandarasi wanatakiwa kutekeleza miradi hiyo kwa muda wa miezi 24.
Hata hivyo alisema wakandarasi hao wamefuata taratibu zote ambazo zilitakiwa kufanyika huku wakiweza kupata wazabuni 16 wa makampuni ya ndani na makampuni mawili tu ambayo ni ya kutoka nje ya nch.
Kwa upande wa wabunge wakizungumza na muda mfupi baada ya kupewa barua ya kuwathibitisha walisema ili miradi hiyo iweze kuteklezeka ni lazima wabunge na wakandarasi wakafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.
Mbunge waKorogwe vijijiniStivine Ngonyani,alisema kuwa ili kuhakikisha miradi ya REA inatekelezeka ni jambo la busala sana wabunge pia wakatoa elimu kwa wananchi juu ya kudai fidia ikiwa ni pamoja kuwapatia ushirikiao wa kutosha.
Tags
umeme wa lea