BANDA MEDIA BLOG

TFDA YAFUNGA BUCHA ZISIZOKIDHI VIGEZO KONGWA

DODOMA: MAMLAKA ya udhibiti chakula vipodozi na dawa TFDA imefungia Machinjio ya Ng'ombe ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuendelea na huduma ya uchinjaji Ng'ombe kutokana na machinjio hizo kutokidhi vigezo vya mlaji.
Kaimu meneja TFDA kanda ya kati Dodoma Dk. Englebert Mbekenga ameeleza kupitia vyombo vya habari kuwa tangu May 12 mwaka huu mpaka watakapofanya marekebisho ndipo watafunguliwa kuendeleza huduma hiyo.
Mbekenga amesema Kwa mujibu wa sheria namba (1) ya mwaka 2003 Ya Chakula Dawa na Vipodozi imeweka wazi kwamba eneo linalohusika na uchinjaji mifugo ili liweze kutambulika kama machinjio inabidi liwe na maji ya kutosha kwa ajili ya kufanya usafi na vyoo vya kutoa huduma kwa wanyakazi wa machinjio.


"Lakini machinjio ya Kongwa haina huduma yoyote ya maji wala bomba na vyoo havina milango hali iliyopelekea utumiaji wa ovyo katika mazingira kwa baadhi ya watu kujisaidia ovyo na uchafu uliokithiri kutokana na ukosefu huo wa huduma ya maji" Mbekenga ameeleza.
Mmoja wa wamiliki wa bucha ambaye pia hutegemea machinjio hayo kwa masharti ya kutotajwa jina alisema kufungwa kwa machinjio hiyo kumeleta ugumu na kuongezeka kwa gharama kwani kwa inawalazimu kusafiri zaidi ya kilometa 16 kupata huduma katika machinjio ya Kijiji cha Mbande.
Na ameiomba serikali kuchukua hatua mapema kufanya matengenezo kwani wao wamekuwa wakilipia kila kichwa kinachochinjwa kiasi cha 3000/= na machinjio hutegemewa zaidi ya Wafanyabiashara hao wa nyama.
Kwa upande wa bei ya nyama ya Ng'ombe Wilayani humo kwa wauzaji waolikuwa wakiuza sh. 4000/= kwa kilo kwa sasa wamepandisha mpaka 5000/= kwa kilo.
Kadhalika Dr Mbekenga ametoa wito kwa wamiliki machinjio binafsi na Halmashauri zote kuhakikisha sheria,kanuni,na taratibu zinafuatwa na TFDA haitarajii kuona nyama safi inatoka katika machinjio zilizilizokithiri kwa uchafu.
Pia ametoa pongezi kwa vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa kwani kupitia habari wananchi watatambua mambo mbalimbali badala ya kubaki gizan

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG