
Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Mh. Augustino Lyatonga Mrema
amewaonya wananchi kuacha kutenda makosa yatakayo wafanya kukataliwa
kurudi kwenye jamii pindi watakapohitaji kupata msamaha 'Parole' na
kusisitiza gerezani siyo hoteli.
Mapema wiki akifanya mahojiano EATV, Mhe. Mrema ameweka wazi kuwa hakuna
mfungwa anayeweza kupatiwa msamaha na bodi ya Parole ikiwa tayari jamii
yake haimtaki na kuongeza kuwa mfungwa atalazimika kutumikia kifungo
chake.
Aidha Mrema ameongeza kwamba watu wamekuwa wakifanya makosa makubwa
kwenye jamii hali ambayo inawanyima nafasi za misamahaa ambayo ni haki
yao na kwamba tatizo linakuja wakati wakupata ruhusa kwa jamii anayoishi
kukataa kutoa ruhusa.
"Huwa tunaauenda eneo analoishi au alipozaliwa kuwaeleza watu juu ya
msamaha wanaotaka kuutoa na kama wakikataa kwa sababu na wao haki yao
kukubali aua kukataa basi mtuhumiwa utarudishwa tu magereza. Nataka
kuwaasa acheni kufanya mambo yatakayowafanya mkatliwe, jiepusheni na
makosa yatakaowafanya mkose haki yenu labda itokee bahati mbaya" Mh.
Mrema alifunguka.
Pamoja na hayo ameongeza kwamba jamii haipaswi kuwakataa watu wao walipo
magereza kwani baada ya kumaliza kifungo watarudi kwenye maeneo yao na
hawatakuwa na uwezo wa kuzuia waendelee kukaa magereza.
"Jamii inatakuwa ifahamu hawa watu waliopo magereza ni bdugu zao na ni
watu wao. Tengezenezeni mahusiano mazuri na siyo kwamba mtu akishafungwa
ndio anageuka mnyama mnatakiwa mtambue ni binadamu na ana haki zake
zote za kimsingi" aliongeza Mrema.
Tags
Augustine Mrema