VIONGOZI wa Kisiasa pamoja na
watendaji wa serikali na taasisi mbalimbali za Umma wametakiwa kuacha
mara moja kuingilia shughuli za kitaalamu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof.Adrof Mkenda alipokuwa akifungua semina ya wakurugenzi wa mipango na sera kutoka Wizara mbalimbali iliyofanyika katika ukutano wa Mikutano wa Hazina Mjini hapa.
Amesema katika kufanya kazi za kutengeneza mipango na sera mbalimbali za kulinda ubora wa mitaji pamoja na usambazaji wa bidhaa ni lazima kujiepusha na matakwa ya wanasiasa ambayo yamekuwa yakiingilia kazi za wataalam.

Prof.Makenda alisema katika kuimalisha ubora wa bidhaa nchini Mamlaka husika zinatakiwa kufanya ukaguzi wa bidhaa huku wakitoa elimu kwa jamii badala ya kutumia mabavu na mashambulio kwa watu ambao wanatoa huduma mbalimbali bila kukidhi viwango.
Amesema katika nchi ya Tanzania kuna sheria ya kufanya biashara hulia lakini hairuhusu kuwa na biashara holela na kueleza kuwa kama biashasha itakuwa holela ni wazi kuwa afya za mlaji zitakuwa mashakani zaidi.
Katika semina hiyo Prof.Mkende amesema katika ukaguzi wa bidhaa ni lazima kujipambanua na kujiondoa katika viashiria vya rushwa ambavyo vinaweza kusabisha kutokea kwa madhara makubwa kwani inapopenyezwa rushwa kunaweza kusababisha kufanyika kwa biashara inayotokana na bidhaa bandia.

“Ebu tujiulize wale askari ambao waliruhusu gari ambalo lilisababisha vifo vya watoto 32 walimu 2 na dereva mmoja wa Shule ya msingi ya Lucky Vicent ya Arusha wamechukuliwa hatua gani?.
“Wakati wakiruhusu gari hiyo hawakuona kama watoto wamezidi katika gari hiyo na walikuwa wamevunja sheria, kwa madhara yaliyotokea ndiyo taswira harisiya kufanya ukaguzi kwa uzembe na kusababisha madhara makubwa ya kuligharimu taifa” alieleza Prof.Mkende.
Katika hatua nyingine Prof.Mkende amesema wenye Mamlaka ya uthibiti wa bidhaa ni lazima nao wakajiweka katika misingi ya kuwa wathibiti bora na siyo wathibiti holela kwa maana ya kuruhusu bidhaa ambazo ni feki kuendelea kutumika na uenda zikasababisha madhara makubwa kwa jamii.

Tags
SIASA