Wanafunzi hao waliochaguliwa ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu.
Hayo yameelezwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,GEORGE SIMBACHAWENE wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Waziri SIMBACHAWENE amesema kuwa wanafunzi hao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka huu,wanatoka kwenye Shule za Serikali na binafsi zipatazo 351 zikiwemo shule 17 mpya ambazo zimepangiwa wanafunzi.
Hata hivyo amebainisha kuwa muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka 2017 utaanza Julai 17 na wasipo ripoti nafasi zao watapewa watu wengine na wale wakidato cha sita masomo yataanza julai 3 mwaka huu.
Tags
ELIMU