Mfungaji
wa mabao mengi nchini Uingereza Wayne Rooney ameamua kustaafu katika
soka ya kimataifa baada ya kukataa kushirikishwa katika kikosi cha timu
ya taifa ya Uingereza kitakachomenyana katika mechi za kufuzu kombe la
dunia.
Mshambuliaji huyo wa Everton
aliombwa na meneja wa timu ya kandanda ya Uingereza kushiriki katika
mechi dhidi ya Malta na Slovakia.
”Kila mara nilipochaguliwa ilikuwa
fahari kubwa kwangu lakini naamini imefikia muda wa kujiondoa” ,
alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alifunga mabao 53 katika mechi 119 za kimataifa.
Rooney ambaye hakushirikishwa na
Southgate katika mechi dhidi ya Scotland na Ufaransa mnamo mwezi Juni
alianza kuichezea Uingereza mwaka 2003 katika mechi ambapo Uingereza
ilipoteza kwa Australia.
Tags
ROONEY