Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evodi Mmanda (mbele) akizungumza na
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara baada ya kuwasili
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kabla ya kuanza kwa ziara katika
miradi mbalimbali ya gesi asilia iliyopo mkoani humo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto mbele)
wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja wa Kiwanda cha
Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo Mtwara, Leonce Mroso (hayupo
pichani) kwenye eneo la kiwanda hicho katika ziara hiyo. Katikati
nyuma ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Jaji Mstaafu, Josephat Mackanja.
Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara
Mtaalam kutoka Kiwanda cha
Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Laurent
Jars (katikati) akielezea shughuli za uchakataji wa gesi zinavyofanywa
na kiwanda hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Mtaalam kutoka Kiwanda cha
Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Nyomwa
Kilemo (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Mtaalam kutoka Kiwanda cha
Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Laurent
Jars (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) kwenye ziara hiyo.
Mtaalam kutoka Kiwanda cha
Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Laurent
Jars (kushoto) akielezea usafirishaji wa gesi asilia kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (kulia) katika ziara
hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (katikati) akionesha wajumbe wa kamati
hiyo sehemu ya eneo la Pwani lililomegwa na maji karibu na Kiwanda cha
Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara kwenye ziara
hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (kulia mbele) akielezea manufaa ya gesi
asilia kwenye uchumi wa mkoa wa Mtwara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti kwenye ziara hiyo.
Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo mkoani Mtwara.
Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata
Gesi Asilia cha Madimba kilichopo Mtwara, Leonce Mroso (kulia) akielezea
matumizi ya gesi asilia kwenye uzalishaji wa umeme kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye eneo la kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (wa tatu kulia mbele) na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili
kulia mbele) wakiongoza wajumbe wa kamati hiyo kwenye ziara katika eneo
la Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo mkoani
Mtwara.
……………………..
Wataalam Madimba watakiwa kuwa wazalendo
Na Greyson Mwase, Mtwara
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia amewataka vijana wanaofanya kazi katika
Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo mkoani Mtwara
kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa weledi, hivyo kuwa na mchango mkubwa
katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta ya gesi.
Ghasia aliyasema hayo kwenye ziara
ya kamati hiyo kwenye miradi mbalimbali ya gesi mkoani Mtwara yenye
lengo la kujionea mafanikio na changamoto zake.
Alisema Serikali imekuwa
ikisomesha vijana katika masuala ya gesi na mafuta, ndani na nje ya
nchi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa sehemu ya umiliki
wa uchumi wa gesi asilia.
Aidha, katika hatua nyingine,
alishauri Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuendelea na
mikakati ya kuwa programu za mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalam hao
kwa kuwa teknolojia inabadilika kila wakati.
“ Vijana wanaofanya kazi nzuri
katika kiwanda hiki ni vyema wakahudhuria mafunzo ya mara kwa mara ili
kuendana na teknolojia inayobadilika mara kwa mara.
Pia alishauri maslahi kwa ajili ya
vijana wanaofanya kazi katika kiwanda hicho yakaendelea kuboreshwa
zaidi ili kuwapa motisha wa kazi zaidi.