Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kuikabili Sumu Kuvu kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania
Bi Eveline Massam wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya Boga kutoka
kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
mara baada ya kutembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya
siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM
Kalangalala Mkoani Geita.
Afisa habari na Uelimishaji Jamii kutoka Mamkaka ya Chakula na Dawa Bi Robert Feruzi (Kulia) akimuelezea Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa jinsi Mamlaka hiyo inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa jinsi Mamlaka hiyo inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo kutoka Benki ya wakulima (TADB) Ndg Joseph Mabula (Kulia) akimuelezea Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (KUshoto) jinsi inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katikanuwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (KUshoto) jinsi inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katikanuwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akionyesha Mvinyo uliotengenezwa na wajasiriamali wadogo wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua mashine mbalimbali katika Banda la kampuni ya POLY MACHINERY CO.LTD kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Na Mathias Canal, Geita
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt
Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo
ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima
nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
Alisema kuwa elimu hiyo inatakiwa
kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini ili wananchi waweze kutambua
namna bora katika uandaaji wa mashamba wakati wa msimu wa kilimo ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha mashamba hayashambuliwi na magugu wala wadudu
waharibifu.
Naibu Waziri ametoa ushauri huo
wakati akizungumza na Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi
ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi
Eveline Massam mara baada ya kutembelea Banda hilo wakati wa Maonesho ya
36 ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika Uwanja
wa CCM Kalangalala Mjini Geita kuanzi Octoba 10 mpaka Octoba 16.
Dkt Mwanjelwa alisema kuwa
wakulima wengi nchini wanalima pasina kufahamu taratibu za kilimo cha
kisasa jambo ambalo linapelekea mazao yao kuathiriwa na wadudu husani
Sumu Kuvu na kupelekea uduni wa mavuno.
Alisema kuwa endapo Taasisi hiyo
ya (IITA) itaongeza nguvu ya utoaji elimu kwa wakulima kwa kushirikiana
na wataalamu wa Wizara ya kilimo, wananchi watanufaika na kilimo chao
ikiwa ni pamoja na kuwa na mavuno mengi.
Alisema Sumu Kuvu inahatarisha
afya za watumiaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara, kwani
chakula na malisho ya mifugo iliyo athiriwa na sumu kuvu hupunguza
uzalishaji huku mazao yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu zaidi ya
kiwango kinachoruhusiwa kutekelezwa au yanauzwa kwa bei ya chini.
Aidha, zipo athari za moja kwa
moja kwani endapo binadamu au mnyama atakula chakula chenye malisho
yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu anaweza kupoteza maisha.
Kwa upande wake Msaidizi wa
Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa
Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam alisema kuwa Sumu
Kuvu huzalishwa wakati fangasi aina ya Aspergillus anaposhambulia mbegu
shambani/ghalani.
Aliongeza kuwa Ukuaji wa fangasi
na athari za sumu kuvu husababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Ukame
wa ongezeko la joto), Mbinu duni za kilimo kabla na baada ya kuvuna
mazao kwa mfano; ukaushaji hafifu wa mazao punde yanapovunwa, na
uhifadhi duni wa mazao ghalani na wadudu waharibifu.
Sumu Kuvu ni aina za kemikali za
sumu zinazozalishwa na aina ya Ukungu au Fangasi wanaoota kwenye mbegu
za nafaka kama vile mahindi, mbegu za mafuta kama karanga, jamii ya
kunde na pia mazao ya mizizi. Pia sumu Kuvu hupatikana katika bidhaa za
mifugo kama vile maziwa, mayai na nyama pale ambapo chakula kinacholiwa
na mifugo kitakuwa kimechafuliwa na sumu hizo.
Sambamba na hayo pia Naibu waziri
wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa alitembelea Banda la Benki ya
Maendeleo ya kilimo, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Banda la
Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Banda la Mamlaka ya chakula na dawa
(TFDA).
Maadhimisho ya Siku ya Chakula
Duniani hufanyika kila mwaka kuanzia Octoba 10 mpaka Octoba 16 ambapo
kwa mara kwanza yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni
ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya miaka 72 ya
kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.
Tags
Nw Mwanjelwa