Meneja Mkuu wa mradi huo, Mhandisi Jiten Divecha ameyasema
hayo Mei 13, 2022 kwa Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa wakati
alipotembelea na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Mgodi wa Kati wa Dhababu wa
Singida (Singida Gold Mine) unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Mining Company
Limited uliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Divecha amesema, kwa sasa mgodi umeendelea kutoa fursa
mbalimbali za ajira kwa Watanzania pamoja na kununua bidhaa za Kitanzania.
Akizungumza, mara baada ya kukagua maeneo ya uchimbaji
katika mgodi huo, Dkt.Kiruswa ameagiza uongozi kuhakikisha wanamaliza
changamoto zote zinazokwamisha kuanza kwa mradi huo ili uchimbaji uanze kwa
haraka.
Amesema, wananchi wa Ikungi na wakazi wa Singida wanatarajia
kuona mgodi huo unaanza kazi ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wa mgodi
katika jamii yao.
Pia, Dkt.Kiruswa ameipongeza Kampuni ya ya Uchimbaji Madini
ya Shanta kwa uwekezaji mkubwa wanaoendelea kuufanya katika mgodi huo ikiwemo
ujenzi wa miundombinu ya mgodi, ajira zinazotolewa, afya na miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Vile vile, Dkt. Kiruswa mgodi wa Shanta kuandaa na
kutekeleza mpango wa uchangiaji wa kampuni yao kwenye jamii (CSR) kwa mujibu wa
Sheria.
Amesema, wanatakiwa kuhakikisha kama wawekezaji jamii
inayowazunguka inanufaika na mradi husika huku akifurahishwa na Sheria ya Local
Content inavyotekelezwa na mgodi huo.
"Nimefurahishwa na mpango wa Local Content, nimetembea
hapa sijaona hata mgeni mmoja, wanaofanya kazi hapa wote ni Watanzania, lakini
pia mnatumia rasilimali zinazopatikana hapa hapa, nimesikia hata maharage
yanatoka hapa,"amesema Dkt. Kiruswa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki,
Miraji Mtaturu amemueleza Dkt.Kiruswa kuwa, wananchi wa Singida wanatamani
mradi huo uanze mara moja ili waweze kunufaika na mradi huo.
Amesema, mradi utakapoanza utaleta maendeleo kwa jamii
inayozunguka pamoja na kuongeza mapato kwa Serikali.
Wengine waliohudhuria ziara ya Naibu Waziri wa Madini ni
viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ikungi, viongozi wa vijiji na kata
wanaozunguka eneo la mradi na wadau wa Sekta ya Madini.