BANDA MEDIA BLOG

No title

 BRELA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUEPUKA MIGOGORO KWAKUIGANA MAJINA

Afisa Utumishi na Utawala wa wakala wa usajili (BERLA) Raphael Mtalima wak 

             NA JOHN BANDA, DODOMA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kurasimisha biashara zao ili kukuza wigo wa shughuli wanazozifanya bila kusababisha migongano ya wenyewe kwa wenyewe unaotoka na kutumia majina yanayofanana.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Utumishi na Utawala wa wakala huo Raphael Mtalima wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambako BRELA inashiriki kwenye wiki ya ubunifu Tanzania MAKISATU

Afisa sheria wa BRELA Cavin Lwambogo akizungumza na wateja

Mtalima amesema wao kama wakala wanashauri kila mfanyabiashara kuhakikisha haigi jina la mfanyabiashara mwenzake na kama ikitokea mtu anataka kusajili jina ambalo tayari walishalisajili awali wanamshauri mhusika kwenda kubadili jina

“mtu akija kusajili jina la kampuni na kwenye mfumo likaonekana jina hilo lilishasajiliwa na mtu mwingine hatuwezi kumsajilia tunamshauri aende kubalisha jina, na hapa nawashauri watu kuyatengeneza majina yao na si kuvamia majina ya watu maana kitendo hicho na sawa na wizi au uporaji”,

Aidha amesema kwa sasa Brela inatoa elimu ya uelewa kwa wananchi ambao wanaishi vijijini kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari vya kijamii kama redia, makongamano, mikutano na maonyesho kama haya ambapo tangu juzi tulivyoanza tunaona mwiitikio ni mkubwa kwa watu kujisajili

Afisa TEHAMA wa BRELA Joram Manyika akiwafafanulia jambo wafanyabiashara

Ameongeza amewakumbusha wafanyabiashara kuendelea kuzihuisha kamapuni zao kila mwaka kutokana na masharti yaliyopo ambayo ni nafuu kuliko kupitiliza mwaka na miaka bila kuzihuisha kwani watapigwa penati za kujitakia  

Amezitaja huduma zinazotolewa na BRELA kuwa ni pamoja na usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Makampuni, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma, utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda, utoaji wa Hataza sanjali na huduma baada ya usajili.

Kisha akazitaja sharia zinazosimamiwa na BRELA kuwa ni pamoja Sheria ya Usajili wa Makampuni Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara Sheria ya usimamizi wa Viwanda Sheria ya Alama za Biashara na Huduma Sheria ya Usajili wa Hataza

   


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG