Askofu Dr. Dickison Chilongani akifafanua ambo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma
Na
John Banda, Dodoma
BANDA
MEDIA ONE.COM
……………………………………………
ASKOFU wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Cetral
Tanganyika na kati (DCT), Dr. Dickison Chilongani
amewataka wanasiasa waliyopo katika nafasi mbalimbali za Uongozi
kujishusha ili kuondoa machafuko yanayoweza kutokea katika kipindi cha Uchaguzi
Ujao wa mwaka 2025.
Dr. Chilongani ameyasema hayo leo Dec 25,2023, wakati akitoa salamu
za Krismasi kwenye ibada iliyofanyika katika kanisa kuu la Roho Mtakatifu
jijini Dodoma, ambapo amesema tatizo la watumishi walio wengi hupenda kujiinua
kutokana na madaraka au fedha walizonazo.
Amesema mwaka 2025, kutakuwa na uchaguzi mkuu wa
kuchagua viongozi wa serikali lakini chakushangaza tayari kampeni mbalimbali ni
kama zimeanza, kuhusu uchaguzi huo, zimeanza kufanyika kama vile uchaguzi huo utafanyika
kesho
“vitimbwi vingi vimeanza, miongoni mwa wanasiasa,
wanasemana vibaya, wanachafuana, wanapigana vijembe na hata pesa zinatunamika
sana, kila mtu anajiinua anajiona yeye ni bora, kila mtu anataka kuwa Rais
mwaka 2025.
“hali hiyo inatokana na wanasiasa walio na viburi
ambao hawawezi kujishusha kutokana na madaraka au fedha walizo nazo, wanajiinua
tena wakitaka kumpita hata Rais Dr. Samia Suluhu Hassan aliyewateua katika
nafasi walizonazo”, amesema
Aidha Askofu huyo amesema hivi sasa kumekuwa na
Wimbi kubwa la watumishi wa Mungu ambao nao wamekua wakijiinua na hata
kujifanya wao ndiyo Yesu.
“sisi watumishi wengine wa Mungu tunajiinua katika
huduma tunazofanya tukitaka kumpita hata
Yesu mwenyewe, ambaye leo tunakumbuka Kuzaliwa kwake, tukisahau Yohana
Mbatizaji alikuwa Nabii Mkubwa, lakini alituachia somo aliposema “mimi nipungue
wewe uongezeke”, akimaanisha Yesu asilinganishwe naye katika utukufu
Alisema hayo akijua yeye hata kama angekuwa na
uwezo wa kufanya chochote lakini isingekuwa sababu ya kumfanya kuwa mkubwa kuliko
Bwana aliyemtuma…
Pia amewaagiza wakristo wa kanisa hilo, kuumbea
uchaguzi ujao wa mwaka 2025, ufanyika vizuri, Amani iwepo na hata watu wasiweze
kuchafuana.
Wakristo Duniani kote leo, Disemba 25,
wamekusanyika katika nyumba za ibada kwa ajili ya kukumbuka Kuzaliwa kwa
mwokozi wao Yesu Kristo, aliyezaliwa zaidi ya Miaka Elfu mbili iliyopita huko
Yerusalem ya Uyahudi…
Waumini mbalimbali wakisalimiana na Mke wa Askofu Chilongani walipokuwa wakitoka kwenye Ibada ya Krismasi
Waumini wa kanisa kuu la Roho Mtakatifu, Anglikana jijini Dodoma Wakifuatilia kwa makini Ibada ya Krismasi iliyoendeshwa na Askofu wa kanisa hilo Dr. Dickisoni Chilongani.
Waumini wa kanisa kuu la Roho Mtakatifu, Anglikana jijini Dodoma Wakifuatilia kwa makini Ibada ya Krismasi iliyoendeshwa na Askofu wa kanisa hilo Dr. Dickisoni Chilongani.