BARAZA LA UUGUZI LAWAITA WATAHINIWA WAOPITISHWA KWENYE MTIHANI
KAIMU msajili baraza la uuguzi na ukunga tanzania Happy Masenga, Akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma hii leo.NA MWANDISHI WETU, DODOMA
BANDA MEDIA ONE.COM
…………………………………………..
KAIMU msajili baraza la uuguzi na ukunga tanzania Happy Masenga amewataka watahiniwa wote waliojisajili kwa ajili ya mtihani wa usajili na leseni kufika katika vituo walivyoomba siku ya kesho Dec 28, 2023 ili kupata maelekezo na namba za mtihani.
Mtihani huo unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Dec 29, mwaka huu, katika vituo vilivyo tambuliwa na kukubalika na baraza hilo, katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Masenga ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa baraza hilo leo Dec 27,2023 jijini Dodoma ambapo amesema watahiniwa hao wanatakiwa kufika na mahitaji yaliyo orodheshwa katika tangazo huku akisisitiza kuwa atakayekosa kufika atakuwa amejikosesha nafasi ya kufanya Mtihani huo.
Katika hatua nyingine Masenga ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wauguzi na wakunga waliopo kazini kuzingatia maadili na kiapo cha taaluma ya uuguzi na ukunga.
jumla ya watahiniwa 4,166 wamekidhi sifa za kufanya mtihani huo wakiwemo 3,917 ambao wanafanya mtihani kwa mara ya kwanza,na 248 wanaorudia.



