DRC: MONUSCO yafunga kambi yake Lubero, Kivu Kaskazini, baada ya miaka 21
Ujumbe huo, unaojulikana kama MONUSCO, umekuwa nchini DRC kwa miongo miwili na uko katika mchakato wa kukamilisha operesheni. Picha MonuscoVikosi vya Umoja wa Mataifa nchini DRC, maarufu MONUSCO
vimefunga rasmi operesheni yao eneo la Lubero, Kivu Kaskazini, mashariki mwa
DRC, baada ya kudumisha usalama eneo hilo kwa miaka 21.
Kufungwa kwa kambi ya Lubero ni katika mchakato mzima wa
kufungwa kwa kambi za vikosi vilizoanzishwa tangu 2021, kutokana na tathmini ya
pamoja ya hali hiyo kutoka kwa MONUSCO na washirika wake nchini DRC.
Josiah Obat, mkuu wa ofisi ya MONUSCO Beni-Lubero,
amesema: "Ujumbe utasalia Beni na, kutoka eneo hili, tutaendelea
kushirikiana na washirika ambao tutaondoka hapa. Mbali na hayo, Mashirika ya
Umoja wa Mataifa yataendelea kuhudumu na idadi ya watu huko Lubero.’’
Hata hivyo, MONUSCO itasalia nchini DRC kubaki hadi 20
Desemba 2024 ikiwa na majukumu muhimu ya msingi yakiwemo kulinda raia, kusaidia
uimarishaji wa sekta ya usalama, na michakato ya kusaidia katika udhibiti wa
silaha.
MONUSCO imejisifia kuwa katika kipindi hicho cha miaka
21, imechangia pakubwa utulivu wa mkoa huo ikiwemo kulinda raia dhidi ya
vitisho kutoka kwa vikundi vyenye silaha na kusaidia miradi kadhaa kwa niaba ya
amani licha ya changamoto tofauti kama vile uwepo wa zaidi ya makundi 40 yenye
silaha katika eneo la Lubero pekee.
