Mauaji Gaza yafikia 21,500 kufuatia mashambulizi ya Israel
Vita vya Israeli dhidi ya Gaza iliyozingirwa vilivyoingia siku ya 84 vimesababisha vifo vya Wapalestina 21,507. / Picha: AA.............................................................................
Takriban Wapalestina 187
wameuawa kwenye mashambulizi ya Israel Gaza ndani ya saa 24 iliyopita, na
kufikisha idadi ya vifo 21,507 tangu Oktoba 7, hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya
Afya katika Gaza.
Wizara hiyo pia imeongeza kuwa
watu 55,915 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita vya Israeli kwenye eneo hilo.
Kulingana na Umoja wa Mataifa
zaidi ya asilimia 80 ya watu milioni 2.4 wa Gaza wamefurushwa makwao, tangu
vita vya kikatili vya Israeli dhidi ya Gaza vilipoanza Oktoba 7.
Israel yawazuia wapalestina
kuingia Msikiti wa Al Aqsa Ijumaa ya 12 mfululizo
Mamlaka ya Israel imewazuia
Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa katika eneo la Jerusalem
Mashariki, hii ikiwa ni Ijumaa ya 12 mfululizo.
Idadi kubwa ya maafisa wa
Polisi wa Israel walitawanywa katika eneo hilo kuzuia waumini kuingia
msikitini, mashahidi waliiambia Anadolu.
Watu walioshuhudia waliongeza
kusema kuwa polisi wa Israeli waliweka vizuizi kwenye milango ya mji wa zamani
na kuruhusu wazee tu kuingia msikiti huo wa Al Aqsa.
Madaktari wasio na mipaka MSF
wasisitiza usitishwaji wa mapigano mara moja Gaza
Shirika la Madaktari wasio na
Mipaka (MSF) wamesisitiza haja ya kusitisha mapigano huko Gaza mara moja.
"Kushindwa kwa Marekani
kuidhinisha mfululizo wa maazimio ya UN yanayotoa wito wa kusitisha mapigano
Gaza kumesababisha kupitishwa kwa azimio llilopunguzwa nguvu ambalo halina
maana kwetu," Jacob Burns, mratibu wa mradi wa MSF huko Gaza, alisema
katika taarifa.
"Vizuizi vya kuleta
misaada kupitia njia ngumu ya vituo vya ukaguzi vya Israeli na Misri ni vya
kweli, lakini kikwazo kikuu kwa wahudumu wetu wa matibabu wanaojaribu kutoa
huduma zaidi na bora ya afya hapa ni kuendelea kwa vurugu," ilisema taarifa
hiyo.
