Mafuriko, maporomoko ya ardhi yaua kadhaa mashariki mwa DRC
Baadhi ya wakazi wakiangalia hasara inayotokana na mafuriko ambayo yanaripotiwa kuuwa watu kadhaa baada ya mvua kubwa iliyonyesha mjini Bukavu, nchini DRC. Picha: ReutersMvua kubwa iliyonyesha usiku
wa kuamkia leo Kusini mwa jimbo la Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo, imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, na kuuwa angalau watu 40,
hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.
Angalau watu 20 wamepatikana
wamekufa katika mji mkuu wa Bukavu huku miili mengine 20 imepatikana katika
kijiji kilichopo karibu na mji wa Burhinyi, taarifa za Jumatano, kutoka ofisi
ya gavana zimesema.
Jitihada za uokozi
zinaendelea, huku kukiwa na wasi wasi wa kuongezeka kwa idadi ya vifo.
Mwezi Mei, mwaka huu, takriban
miili 438 ilipatikana katika maeneo ya Kalehe, Kusini mwa Kivu eneo lililopata
athari kubwa ya mvua.
DRC, mara kwa mara inakabiliwa
na majanga ya asili katika msimu wa mvua.
