Rais wa Zambia Hichilema asamehe wafungwa 588
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesamehe wafungwa 588 katika magereza mbalimbali ya nchi.
Miongoni mwa wafungwa
waliosamehewa ni pamoja na wazee 11 na mama mwenye mtoto, vyombo vya habari vya
ndani vimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ulinzi Jack Mwiimbu.
Kifungo cha maisha
kimepunguzwa hadi miaka 35 na wafungwa wawili ambao awali walihukumiwa kifo
hivi sasa watafungwa maisha, waziri aliwaambia waandishi wa habari mjini Lusaka
siku ya Jumapili.
Kusamehewa kwa wafungwa na
Rais Hichilema ilikuwa ni utekelezaji wa kifungu nambari 97 cha katiba ya nchi
ambacho kinampa rais mamlaka ya kusamehe au kubadilisha adhabu iliyowekwa kwa
wafungwa, amesema Waziri Jack Mwiimbu.
Amesema msamaha huo umeonyesha
tabia nzuri baada ya wafungwa kujirekebisha tabia ambayo itawasaidia kujumuika
na jamii.
