Padri Felix Francis Akimbatiza Moja wa Watoto hao waliobatizwa katika kigango cha Mtakatifu Ambloce Iyumbu jijini Dodoma...
…………………………………………
NA JOHN BANDA, DODOMA
BANDA MEDIA ONE.COM
WAZAZI na walezi wameaswa kuwalea watoto wao katika
maadili mema tangu wanapokuwa na umri Mdogo badala ya kusubiri kuwakabidhi walimu
wakawafundishie pindi wanapowaandikisha shuleni…
Kauli hiyo imetolewa leo Disemba 26,2023 ambayo ni
siku ya Kufungua zawadi (BOXING DAY) na Padri Felix Francis wakati alipokuwa
akiongoza Ibada ya Ubatizo katika Kigango cha Mtakatifu Ambloce kilichopo
iyumbu Jijini Dodoma
“Steling Bora kwenye Muvi ya Maisha hutengenezwa
kuanzia nyumbani, siku zote mtoto alivyo ndivyo familia ilivyo, ukiona mtoto
anakata mauno hovyo kwenye michezo yake ujue wazazi hawamkemei wala kumkataza
kitu”,
Amesema wazazi wasione kuwa hao ni watoto wadogo na
kwamba wakiwakataza jambo ambalo wanaona ni baya basi wataonekana hawawapendi.
“hao ambao ninyi leo mnaona ni watoto mkiwaacha
kufanya, kusema na kucheza kila aina ya michezo wanayo iona kwenye TV, Kesho
wanapoonza shule hayohayo wanaenda kuyaonyesha kwa wenzao.
Mfano miongoni mwa wanafunzi shuleni kwangu, wakati
furani nilimshuhudia mmoja akicheza mchezo wa uvunjifu kabisa wa maadili,
nilipomuita mzazi wake na kumueleza akahamaki kisha akasema mbona kukata Viuno
ni jambo la kawada tu, hata kwenye tv watoto wanaona”,
Padri huyo anasema ikabidi atumie Busara ya
kumruhusu Yule mama aondoke, lakini kabla ya kuondoka “nikamwambia aniachae
mtoto nitamfundisha na kumwekeza mwenyewe, “fikili kidogo, kama mzazi anajibu
hivyo je ukimuachia mtoto kwa kumfukuza shule si ndiyo ataenda kuharibika
kabisa?’’, amesema na kuoji
Aidha amesema wazazi na walezi wengine hata
wakielezwa kuhusu namna ya kuwasaidia watoto wao katika malezi bora, wanakuja
juu, “niwaambie sisi walimu tunajua jinsi familia zinavyoishi kupitia watoto
wao, maana Nyumbani ndiko picha linapoonzia Steling hutengenezwa kuanzia nyumba”,
amesema Padri huyo wa shirika la Don- Bosco ambaye kwa sasa anafanyia kazi huko
mkoani Shinyanga…
Jumla ya Watoto 8, kutoka katika familia tofauti
leo wamebarikiwa na kubatizwa wakikaribishwa katika kundi la washirika wa
kanisa hilo ambapo wazazi, walezi na wasimamizi wao wamesisitizwa kuwa karibu
nao na kwa kuwalea katika maadili ya Kikristo mpaka pale watakapokuja kujitegea
wenyewe .
Ubatizo Ukiendelea