Wananchi wa Mtaa wa Itega Shina namba 2 wakiangalia tingatinga lililokuwa likichonga Barabra ya Mantoga,
Diwani wa Kata ya Nkuhungu Daid Mkandi akiwa katika picha pamoja na wakazi wa mtaa wa Mantoga wakati zoezi la kuchonga barabara ya mtaa huo likiendelea.
NA JOHN BANDA, DODOMA
WAKAZI wa Mtaa wa Itega Kata ya Nkuhungu jijini
Dodoma wamekuwa Tofauti na wakazi wa
maeneo mengine hapa nchini ambao wamekuwa wakiilalamikia Serikali kuhusu
maswala ya Utengenezaji wa miundombinu hasa ya barabara ambapo wao wameamua kuchangishana fedha na
kufanikisha uchongaji wa barabara yenye urefu wa mita 250.
Akiongea mbele ya Camera za waandishi wa habari
katika Barabara hiyo ya Mantoga shina namba 2, leo Januari 16,2024 Ashiru Lumato
ambaye ni mkazi wa mtaa huo amesema kutokana na Adha kubwa ambayo wamekuwa
wakioipata ya magari kushindwa kupita kutokana na maji mengi kutuwama na
kutengeneza tope la mfinyanzi waliamua kuitana wakakubaliana kisha wakaanza
kuchangishana fedha kwa ajili ya kuondoa kero hiyo.
“kazi hii inayoendelea kufanyika ni nguvu zetu
wenyewe, tulijikusanya wakazi wa mtaa wetu tukakubaliana kuchangishana fedha
tukapata million 2.4 na ndizo
zimefanikisha zoezi hili”, amesema
Kwa Upande wake Katibu wa Shina namba 2 katika mtaa
huo Asha Sengoli, amesema wakazi hao walifikia maamuzi hayo kutona na kuona kuwa
kama wataisubiri serikali kuja kuwachongea barabara hiyo watachelewa huku wao wakiendelea kuteswa na
ubovu wa barabara hiyo iliyo katikati ya makazi ya watu.
Katibu mwenezi wa CCM, Tawi la Itega Zena Legu
amesema wao kama chama walishirikishwa na hivyo na wao kuwaunga mkono kwa
kuwachangia 150,000 kwa ajili ya kufanikisha mpango wao.
Diwani wa
Kata ya Nkuhungu Daudi Mkandi amewapongeza wananchi wa mtaa huo kwa maamuzi
hayo ya ujasili na Moyo wa Kujitolea kwa Nguvu na mali zao,
“nawapongeza wananchi kwa Kuchangia Fedha na kujitolea
kwa Nguvu zao katika kufanikisha zoezi hili, nimeambiwa pia kuna mkazi mmoja wa
mtaa huu ni Mhandisi na ndiye aliyetoa mitambo hii ya uchongaji na magari ya
kumwaga vifusi ambapo fedha zaidi ya million 2.6 zilizochangwa zimetumika
kununulia mafuta
Aidha Diwani huyo aliwashauri Viongozi wa Mitaa na Kata nyingine kuwashirikisha wananchi wa maeneo yao katika shuhuli za maendeleo kwa kuwahamasisha badala ya kubaki wakiisubiri serikali peke yake.