Simba Wamemuenzi Hayati Mzee Mwinyi (Mzee wa Rukhsa), Rais wa Awamu ya Pili, wamefanya hivyo kwa ushindi mnono wa goli 6-0 na kutinga robo fainali.
Simba Ambayo ilichabangwa Magoli 2 .0 na Boll Zozo wa Stella Club d' Adejame' ya Ivery Cost Mwaka 1993, katika Ardhi ya Tanzania kwenye mashindano kama haya, Wakati huo Mzee Mwinyi akiwa Rais na Mgeni Rasmi kwenye Mchezo huo.
Tunaweza kusema kilichoiponza Jwaneng Galaxy ni maneno ya Kocha wake Morena gubu kutokana na maneno mengi ya kutisha kuliko uzito wa jeshi lake uwanjani, hawakuwa na uwezo hata punje wa kujibu maswali ya Mnyama walipiga kila goti mbele ya Simba hadi dakika ya mwisho.
nakumbuka alisema Simba wazee but yeye anapaswa kuanza kuacha vijana magalasa anaomiliki kabla ya Simba kuacha wazee
Chama ni mmiliki wa Game nzima hakika ni mechi yake na amemudu mambo mengi kiwanjani kama si kukosa bahati angeondoka na Hat Trick, Benchikha alimtuma kazi ya Zidane ya mwaka 1998 mbovu mpe ataboresha nzima mpe itakuwa hatari zaidi.
Heshima ya nchi imelindwa kwa mara ya kwanza Tanzania inaingiza timu mbili kwenye robo fainali wakati mataifa mengine yakiingiza timu moja moja hakika ni hatua kubwa katika soka la Tanzania na Mzee wa Rukhsa ambaye alikuwa shabiki wa Mnyama amernziwa siku ya kupumzishwa kwake malaloni.
