BANDA MEDIA BLOG

RC SENYAMULE AWATAKA MADEREVA BAJAJ NA BODABODA KUWA WAAMINIFU NA WAADILIFU KWA ABIRIA WA TRENI YA MWENDO KASI

 

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akibandika bango la kuhamsisha maonyesho ya Nanenane yanayotarajiwa kufanyika kuanzi julai 31 mpaka agosti 9 mwaka huu jijini humo.

                            ..............

                NA JOHN BANDA, DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule leo amekutana na madereva wa Bajaji  na Bodaboda maarufu Maafisa Usafirishaji na kuwataka kuwa waaminifu na waadilifu wakati wa kutoa huduma hiyo Muhimu kwa abiria watakao letwa na Treni ya Mwendo kasi na wa maonyesho ya Nanenane yakayofanyika mkoani humo Kitafa na Kamataifa.

Senyamule ameutoa ushauri huo wakati wa uzinduzi wa  Kampeni na Hamasa, kuelekea Maonyesho ya Nanenane ambayo yatafanyika jijini humo Kitaifa huku nchi kadhaa zikiwa zimeahidi kushiriki, na kwamba ofisi ya Mkuu wa Mkoa imewashirikisha Madereva hao kutangaza na kuhamasisha maonyesho hayo kwa njia ya mabango yatakayobandikwa kwenye Bajaji


Amesema kutokana na abiria wengi wageni kutoka ndani na nje ya nchi na wale wa mkoani Dodoma watakaoshiriki kwenye maonyesho ya Nanenane madereva hao wahakikishe wanakuwa waadilifu na waaminifu.

“ili huduma za usafisha ziendelee kunoga nataka kila mmoja wenu  awe muadilifu na mwaminifu”, amesema

 Aidha amesema maonyesho hayo yatakuwa ya siku 10 yakitarajiwa kuanza Julai 31, mpaka Agosti 9 mwaka huu,

Akizungumzia Treni ya Mwendo kasi mabayo itaanza kutoa huduma za usafirishaji kuanzia hapo kesho kutoka Dodoma kwenda mkoa ya Morogoro na Dar es laam amesema itazinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ambaye ataingia jijii humo kwa usafiri huo na kwamba uzinduzi utafanyika agosti 1, mwaka huu na kuwataka kushiriki kumpokea.   

Pia amewaahidi Madereva hao kuwa Mwisho wa mwezi wa 8 atakutana  nao kwenye kikao cha Pamoja,

“Jiandaeni kwenye kikao hicho kitatumika kusikiliza kero zenu, tutazijadili na kuzitafutia ufumbuzi, pia sisi kama makao makuu lazima tuwe tofauti hata kwa kuvaa sare zitakazotutofautisha na madereva wa mikoa mingine.

Bodaboda na bajaji ni chanzo sahihi cha ajira kwa vijana, Rais ametuelekeza kuwatengenezea mazingira salama yatakayowawezesha kufanya shughuli zenu kwa amani na utulivu,

Mwenyekiti wa Chama cha Bodaboda na Bajaj  Mkoa wa Dodoma (UPAMDO)  Chacha Marwa, Ameushukuru Ungozi wa Mkoa huo, Kwa kulikukumbuka kundi hilo linalotoa huduma ya usafirishaji na kulishirikisha kwenye uzinduzi huo wa matangazo na hamasa kuelekea Maonyesho ya Nanenane yanayotarajiwa kufanyika jijini humo

“tunaishukuru serikali ya mkoa wetu kutukumbuka na kuona umuhimu wetu na kuamua kutushirikisha katika uzinduzi huu ambao unatupa nafasi ya kufanya kazi na ofisi ya mkoa kutangaza na kuhamasisha maonyesho ya Nanenane,

Pia tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutujali na kutuletea Treni ya Umeme ambayo inatarajia kuanza shughuli za usafirshaji kuanzia kesho julai 25,2024 Dodoma mpaka Dar es laam, ambayo itatupatia fursa kubwa ya kupata abaria wa kutosha hali itakayotuinua kiuchumi”, amsema

Aidha ameahidi kuwa kundi hilo litaendelea kuiunga mkono serikali kwa shughuli zake za maendeleo kila watakaposhirikishwa kufanya hivyo.  









Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG