Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kutokuwa samaki badala yake akawe kiongozi ambaye yuko tayari kujifunza kwa wale ambao wanamzunguka ili kufikia lengo la kuwatumikia Watanzania.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Agosti 29, 2026, kwenye hafla ya uapisho wa Ndejembi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma huku akisisitiza kuwa Watanzania wana matarajio makubwa kwake.
Pia Rais Samia amelishukuru Bunge chini ya Spika Mussa Azzan Zungu kwa kumpitisha kushika wadhfa huo kwa kura 324 sawa na asilimia 100. Nafasi hiyo iliachwa wazi na Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye alipoteza sifa za kuendelea na wadhifa huo.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azungumza katika Uapisho wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius John Ndejembi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Tags
MAKAMU WA RAIS






