Mchungaji Mahenge amemtaja Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Danken Boaz kuwa ni mwimbaji wa kupigiwa mfano na waimbaji pamoja na watumishi wengine wa Mungu kwa Kutoyazoea Madhabahu.
Mahenge anasema huko jijini mwanza akiwa Mchungaji katika idara ya maombi ndani ya kanisa ambalo Danken Boaz alikuwa akisali, ndipo alipogundua nidhamu ya pekee ya mwimbaji huyo, aliyekuwa akifanya maombi kwa muda wa ziada akiombea nyimbo atakazoongoza kwenye ibada itakayofuata, hata baada ya wenzake kuondoka kanisani hapo.
"Danken ameyakataa mazoea, amekuwa na nidhamu kubwa na madhabahu kwa kila anachokiimba hutumia muda mwingi kukiombea ili kikawaguse wasikilizaji wake", amesema
Aidha Mchungaji Mahenge akatumia nafasi hiyo kuwashauri waumini hapa nchi kuikataa Roho ya Mazoea wakati wa Ibada na hata katika maisha yao kwa ujumla, akiwataka kila wanachokifanya wakifanye kwa kumaanisha.
