Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndugu *Pili Mbanga*, tarehe 26 Oktoba 2026, amefanya mkutano wa ndani katika Kata ya Hanethi, Kijiji cha Humekwa,na Kijiji cha Chenene Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino.
Katika mkutano huo, Katibu wa CCM Mkoa amewaomba wananchi kumchagua mgombea wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Netho Ndilito,pia amewaomba Wananchi wa Vijiji hivyo kujitokeza kwa Wingi kupiga kura ifikapo tarehe 4 Nov 2026.
Aidha ameeleza maendeleo yaliyofanyika na yatakayo fanyika katika vijiji hivyo kupitia serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwani tukimchagua Mgombea Dkt Netho Ndilito atahakikisha anaendeleza kazi na juhudi za maendeleo zilizoachwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Deogratius John Ndejembi, kwa kushughulikia changamoto za wananchi na kusimamia maendeleo ya Chamwino.
*kauli Mbiu :Nipitie tukatick CCM*💚💛 ✅










