KATIKA Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Oktoba 25,2026, kumefanyika Ibada Takatifu ya Kuamuru kwa Daraja Takatifu la Ukasisi, Ibada Hiyo Imefanyika katika Kanisa Kuu la Watakatifu Wote, ambayo iliongozwa na Askofu wa Dayosisi hiyo Luzineth Kingamkono. ambapo watumishi wawili Dkt. Faith Ndugai na Ruth Mbenah ambapo pia wametangazwa kuwa Ma Canon wa Heshima
Katika Tukio hilo lililofanyika kwenye Ibada ya Kuhitimisha Sinodi ya 12 iliyofanyika kanisani hapo kwa siku Tano mfululizo huku mnenaji akiwa, Askofu Moses Yamo wa Dayosisi ya Rorya huko mkoani Mara, ambapo kwenye mahubiri ya kuhitimisha amewataka Makasisi na watumishi ngazi mlimbali wa kanisa hilo, kuzitambua Fursa na kuzitumia ili kuleta mabadiliko katika Parishi zao bila kuogopa mazingira.
Aidha amewataka kuwa wabunifu, wanye kushirikiana na kutumia tekinolojia kupitia Mitandao ya kijamii kuieneza Injili ya Yesu ili kuwafakia watu wengi zaidi.
"mnawafikiaje watu waliopo majumbani, undeni Makundi Sogozi (whatsup group) na mitandao mingine ya kijamii watumishi wekeni huko mahubiri, pia kuweni wabunifu, wewe mchungaji kila siku sauti yako madhabahuni hutaki kualika wala kushirikiana na wenzako waje kenye ibada zako kuhubiri watu watakuchoka", amesema na kuongeza
Kwa Upande wake Askofu wa Dayosisi hiyo Luzineth Kingamkono, akiwaapisha Dkt. Ndugai na Ruth Mbenah kushika nafasi hizo Amewataka kuwa watii na wenye shukurani, wasio kosa wenyewe wala kuwakosesha wengine katika huduma hiyo kubwa na Takatifu.











