Rais wa Mother's Union Duniani Kathleen Snow akimkumbatia Mwenyekiti wa UMAKI Tanzania, Rhoda Kijumbe wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa UMAKI Kasisi Margaret Ndonde na Mkurugenzi wa Mipango Sarah Newnham
RAIS wa Mother's Union Duniani Kathleen Snow akifurahia jambo pamoja na mwenyeji wake, alipowasili Uwanja wa Ndege jijini Dodoma
NA JOHN ISRAEL, BANDA MEDIA- DODOMA
RAIS wa Mother's Union Duniani Kathleen Snow Amewasili Nchini Tanzania na Moja kwa Moja akaelekea Mkoani Dodoma akitokea, Nchini Uingereza ambapo awali alikuwa Durban Nchini Africa ya Kusini kushiriki Kongamano la maadhimisho ya miaka 150 ya Umoja wa Kina Mama (MOTHER'S UNION) lilifanyika pamoja na mkutano mkuu, ambapo Kina Mama zaidi ya Elfu 2, wa Asili ya Kanisa la Anglikana Toka katika mataifa mbalimbali, walishiriki mada mbalimbali pamoja na kusheherekea wakimtukuza Mungu kwa nyimbo na Neno.

Ikiwa ni Msimu wa Maadhimisho hayo ya Miaka 150 ya Mother's Union Bi. Snow aliyeongozana na Mkurugenzi wa Mipango wa Umoja huo Sarah Newnham wametua Nchini kwa lengo la Kutembelea na Kujionea Shuhuli mbalimbali za kina Mama zinazoratibiwa na kutekelezwa na Idara ya UMAKI ya Kanisa Anglikana jimbo la Tanzania kupitia mradi wa Mchakato wa Uhamsishaji wa Kanisa na Jamii katika swala la Maendeleo (CCMP)

Katibu wa Umoja wa Kinamama wa Kikristo Tanzania (UMAKI) anayeratibu Shuhuli zinazotekelezwa na umoja huo, Mchungaji Margaret Ndonde amesema wageni hao akiwemo Mchungaji Mercy Muriithi, ambaye ni Mkuu wa Kanda D kutoka nchini Kenya, watakuwa DCT Oktoba 11,2026 kisha wataelekea Dayosisi ya Rift Valley (DRV) ambapo pamoja na mambo mengine wageni watatembelea baadhi ya vikundi vya kuweka na kukopa na baadae Oktoba 13 watashiriki kwenye maonyesho ya vikundi zaidi ya 29 vya Akiba na Mikopo vinavyowezeshwa na kanisa Anglikana Tanzania kipitia mradi wa CCMP huko maweni wilayani Manyoni Mkoani Singida

Njua Kiswahili Kidogoo ni kauli aliyoitoa Mkurugenzi wa Mipango wa Mother's Union Sarah Newnham wakati akitoa salamu katika wanja wa Ndege jijini Dodoma
Mke wa Askofu WA DCT, Pendo Chilongani akimkaribisha Rais wa Mother's Union Duniani Kathleen Snow alipowalisi jijini Dodoma
