BANDA MEDIA BLOG

MASHAMBULIZI YA UGAIDI JIJINI PARIS YAMTISHA DAVID LUIZ KUREJEA UFARANSA


Nyota wa Paris Saint-Germain, David Luiz hataki kurejea katika klabu yake kufuatia matukio ya mashambulizi ya kigaidi Jijini Paris yaliyouwa watu 129 na kuishtua Ufaransa na dunia nzima.

Luiz, ambaye yupo katika majukumu ya kimataifa na timu ya Brazil, anatarajiwa kurejea Ufaransa baada ya mchezo wa kuwania kufuzu kutinga fainali za Kombe la Dunia katika mchezo dhidi ya Peru jumanne.

Hata hivyo beki huyo aliyesajiliwa na Paris Saint-Germain kwa kitita cha paundi milioni 50 akitokea Chelsea anaonyesha kusita kurejea Ufaransa kutokana na kuhofia usalama wa familia yake na marafiki Jijini Paris.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG